Ilani ya Faragha kuhusu Ukusanyaji wa Rekodi za Sauti kutoka kwenye Vipengele vya Watoto katika programu ya Mratibu wa Google
Tunataka kuwasaidia wazazi waelewe jinsi tunavyokusanya maelezo ya sauti na matamshi wakati watu wanatumia vipengele vya watoto, kama vile Vitendo vya Familia kwenye Mratibu wa Google au video za YouTube Kids, kupitia programu ya Mratibu wa Google. Kando na maelezo yaliyotolewa kwenye Sera ya Faragha ya Google Ilani hii ya Faragha inazingatiwa pia kwenye matumizi ya vipengele hivi katika programu ya Mratibu wa Google.
Watoto ambao hawajafikisha umri unaoruhusiwa katika nchi ambako wazazi wao wamefungua Akaunti ya Google kwa kutumia Family Link wanaweza kuunganisha akaunti zao kwenye vifaa vingi vilivyo na programu ya Mratibu wa Google. Chaguo la "Jumuisha rekodi za sauti" chini ya mipangilio ya Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu hudhibiti iwapo rekodi za sauti na matamshi zitahifadhiwa katika Akaunti yako ya Google unapotumia sauti yako kuwasiliana na programu ya Mratibu. Chaguo hili limezimwa kwa chaguomsingi wakati unafungua Akaunti ya Google na halihitajiki ili utumie programu ya Mratibu. Iwapo chaguo la "Jumuisha rekodi za sauti" chini ya mipangilio ya Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu limeteuliwa katika akaunti ya mtoto wako, anapotumia programu ya Mratibu kwenye kifaa alichotumia kuingia katika akaunti, huenda rekodi ya utumiaji wake pamoja na maudhui ya sekunde chache kabla, ikahifadhiwa katika akaunti yake.
Ikiwa umemfungulia mtoto wako akaunti mpya kwa kutumia Family Link, unaweza kufikia, kusasisha, kuondoa na kuhamisha rekodi za sauti za mtoto wako kwa kuingia katika Akaunti yake ya Google. Ikiwa umesahau nenosiri la akaunti ya mtoto wako, unaweza kuliweka upya kupitia programu ya Family Link au kupitia mipangilio ya Family Link kwenye wavuti. Baada ya kuingia katika akaunti, unaweza kutumia vidhibiti mbalimbali vilivyobainishwa kwenye Sera ya Faragha ya Google (kama vile Vidhibiti vya shughuli kwenye Google) ili udhibiti mipangilio ya rekodi ya sauti ya mtoto wako na rekodi za sauti zilizohifadhiwa katika akaunti yake, ikiwa ni pamoja na kufuta shughuli zozote zilizohifadhiwa kwenye akaunti yake.
Ikiwa mtoto wako alifungua akaunti yake mwenyewe kabla ya kubadilishwa kwa umri wa chini zaidi unaoruhusiwa katika nchi uliko na baadaye ukampa ruhusa ya kuendelea kutumia akaunti hiyo, huenda ukahitaji ruhusa ya mtoto wako ili ubadilishe nenosiri lake au uingie katika akaunti yake.
Iwapo unatumia vipengele vya watoto—kama vile Vitendo vya Familia kwenye Mratibu wa Google au video za YouTube Kids—katika programu ya Mratibu wa Google bila kutumia Akaunti ya Google Inayodhibitiwa kupitia Family Link ambayo imechagua kuweka rekodi za sauti, tutakusanya tu kwa muda mfupi rekodi za sauti na matamshi za matumizi hayo. Maelezo haya huchakatwa ili kuruhusu utumiaji wa kipengele cha sauti, ili tuweze kutoa huduma kwa ufanisi kisha tunayafuta mara moja.
Yalisasishwa mara ya mwisho: tarehe 2 Septemba, 2021